Jumatatu, 10 Oktoba 2016

Mkuu wa Wilaya azindua kampeni ya Mti wangu.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa amezindua siku ya upandaji mti Kiwilaya ambapo Kimkoa ilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa na kauli mbiu "MTI WANGU"

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imepanda jumla ya miti 1650 na zoezi hili ni endelevu lengo likiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Stephen Katemba siku ya upandaji mti" MTI WANGU"

Jumapili, 9 Oktoba 2016

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar Es Salaam Isaya Mwita  (wa kwanza kulia) akipanda mti katika eneo la daraja la Mwalimu Nyerere siku ya upandaji mti

Mbunge wa Kigamboni Mhe. Faustine Ndungulile akimwagilia mti alioupanda siku ya Upandaji mti huku akishuhudiwa na watumishi wa Halmashauri ya Kigamboni na wananchi

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni  Bw. Hashim Mgandilwa akipanda mti wake

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Bw. Stephen Katemba akimwagilia mti wake 

Pamoja tunaweza 

Watumishi wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya Bw. Hashim Mgandilwa na Mkurugenzi wa Halmashauri Bw. Stephen Katemba siku ya kupanda miti. 

Mbunge wa Kigamboni Mhe. Faustine Ndungulile akiwasalimia wananchi waliojitokeza kupanda miti

Alhamisi, 6 Oktoba 2016

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Bw. Stephen Katemba akiongea na halaiki cku ya upandaji mti(Mti wangu) eneo la Daraja la Mwalimu Nyerere. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Halmashauri Bibi Rachel Mhando