Ijumaa, 23 Desemba 2016

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa ametembelea miradi ya maendelea katika kata mbalimbali na kutoa ushauri na kushiriki katika Ujenzi.

Mkuu wa Wilaya Mhe. Hashim Mgandilwa akijaza kifusi katika ujenzi wa darasa shule ya Msingi Kisiwani

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa (watatu kushoto) akikagua miradi

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa akikagua ujenzi wa choo katika shule ya Sekondari Mianzini

MKUU WA WILAYA YA KIGAMBONI AONGEA NA WATUMISHI 


Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa ameitisha kikao cha watumishi kwa lengo la kujitambulisha pia kuwaasa watumishi wafanye kazi kwa bidii.

Akiongea na watumishi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni aliwapongeza watumishi kwa kuanzisha Halmashauri mpya pia kasi walioanza nayo waendelee nayo.

''Nawapongeza sana kwa kuchaguliwa kuja Kigamboni. Fanyeni kazi, taarifa zitolewe kwa wakati na kazi zifanyike. Kama huna jibu la swali la mteja mwambie ukweli na si kumsumbua au kumdanganya.Fanyeni kazi, acheni mambo ya kukaa ofisini, tokeni nje ili kujua shida za wananchi'' Alisema Mgandilwa.

Pia alisema kuwa Kigamboni ni eneo pekee katika Jiji la Dar es Salaam linaloendelezwa, hivyo kuna haja ya kupanga vizuri. Aliwaagiza watumishi wa ardhi  kusimami, kuzuia migogoro ya ardhi na kuuza kiwanja kwa watu wawili tofauti.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Bw. Stephen  E. Katemba

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa akiongea na watumishi (hawapo pichana)

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni  Bw. Hashim Mgandilwa (wakwanza kulia) akifuatiwa na Katibu Tawala wa Wilaya Bibi Rachel Mhando  na Kaimu Mkuu wa Idara ya  Utumishi na Utawala Bibi Paulina Siara   

Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni wakiwa kwenye mkutano wa Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya (hawapo pichani)

Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri (hayupo pichani)