Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Kigamboni Ndg. Stephen Katemba pamoja na Mtendaji mkuu wa wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) Ndg Eliud Mwakalinga wametia saini ya mkataba wa ujenzi wa ofisi
ya Halmashauri ya Manispaa kuanzia Januari 2018.Ujenzi huo wa ofisi unatajiwa
kuchukua miezi Minane na unatarajiwa kukamilika mwezi wa tisa mwaka 2018.
Kukamilika kwa ujenzi huo kutaondoa usumbufu kwa watumishi na wananchi wanaofika kupata huduma kutokana na ofisi za Idara mbali mbali kuwa sehemu tofauti tofauti hivyo kuwalazimu wananchi na watumishi kusafiri toka ofisi moja kwenda nyingine.
Kwa upande wa rasilimali ,Halmashauri itaokoa zaidi ya shilingi milioni 30
zinazotumika kulipia ofisi za Manispaa katika majengo ya watu binafsi kwa
Mwaka.Mtendaji mkuu wa TBA Ndg. Mwakalinga alimuhakikishia Mkurugenzi kuwa
wanakabidhi jengo kwa muda waliokubaliana kwenye mkataba.Kukamilika kwa ujenzi huo kutaondoa usumbufu kwa watumishi na wananchi wanaofika kupata huduma kutokana na ofisi za Idara mbali mbali kuwa sehemu tofauti tofauti hivyo kuwalazimu wananchi na watumishi kusafiri toka ofisi moja kwenda nyingine.