Mkuu wa Wilaya Mhe. Hashim Mgandilwa akijaza kifusi katika ujenzi wa darasa shule ya Msingi Kisiwani |
Ijumaa, 23 Desemba 2016
MKUU WA WILAYA YA KIGAMBONI AONGEA NA WATUMISHI
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa ameitisha kikao cha watumishi kwa lengo la kujitambulisha pia kuwaasa watumishi wafanye kazi kwa bidii.
Akiongea na watumishi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni aliwapongeza watumishi kwa kuanzisha Halmashauri mpya pia kasi walioanza nayo waendelee nayo.
''Nawapongeza sana kwa kuchaguliwa kuja Kigamboni. Fanyeni kazi, taarifa zitolewe kwa wakati na kazi zifanyike. Kama huna jibu la swali la mteja mwambie ukweli na si kumsumbua au kumdanganya.Fanyeni kazi, acheni mambo ya kukaa ofisini, tokeni nje ili kujua shida za wananchi'' Alisema Mgandilwa.
Pia alisema kuwa Kigamboni
ni eneo pekee katika Jiji la Dar es Salaam linaloendelezwa, hivyo kuna haja ya
kupanga vizuri. Aliwaagiza watumishi wa ardhi
kusimami, kuzuia migogoro ya ardhi na kuuza kiwanja kwa watu wawili
tofauti.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa |
Jumatatu, 10 Oktoba 2016
Mkuu wa Wilaya azindua kampeni ya Mti wangu.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imepanda jumla ya miti 1650 na zoezi hili ni endelevu lengo likiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa amezindua siku ya upandaji mti Kiwilaya ambapo Kimkoa ilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa na kauli mbiu "MTI WANGU"
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Stephen Katemba siku ya upandaji mti" MTI WANGU" |
Jumapili, 9 Oktoba 2016
Alhamisi, 6 Oktoba 2016
Jumatatu, 12 Septemba 2016
Mkuu wa Wilaya akiongea na jumuia ya Mtaa wa Feri (Tandavamba)
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa amefanya mkutano na wamiliki wa Boti,wavuvi, mafundi friji,mafundi mashine za boti,mama lishe, wafanya biashara wa vioski, wauza maji na kahawa wa mtaa wa Feri (Tandavamba), lengo kuu likiwa ni kujitambulisha. Kutokana na mazingira mabaya ya sehemu wanayojipatia riziki umoja huo, Mgandilwa aliahidi kuwa litajengwa Soko la Kimataifa la Samaki ambalo pia litakuwa chanzo kikuu cha mapato katika Wilaya ya Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya ya
Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa akiongea na wakazi wa mtaa wa Feri - Tandavamba
|
Mkurugenzi akiwa Tandavamba
Diwani wa Kata ya Kigamboni
Utambuzi wa Mipaka ya Soko la Urassa
Jumapili, 11 Septemba 2016
Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Stephen Katemba(hayupo pichani) wakati akijitambulisha.
Ijumaa, 2 Septemba 2016
Jumatatu, 29 Agosti 2016
Jumatatu, 15 Agosti 2016
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni wametembelea kituo cha kulea wazee wasiojiweza kilichopo Nunge katika Wilaya ya Kigamboni.Wakiwa kituoni hapo walizungumza na wazee waliopo katika kituo hicho na kutoa onyo kali kwa wale ambao huuza vitu wanavyopewa kama msaada kituoni hapo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)