Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa ameitisha kikao cha watumishi kwa lengo la kujitambulisha pia kuwaasa watumishi wafanye kazi kwa bidii.
Akiongea na watumishi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni aliwapongeza watumishi kwa kuanzisha Halmashauri mpya pia kasi walioanza nayo waendelee nayo.
''Nawapongeza sana kwa kuchaguliwa kuja Kigamboni. Fanyeni kazi, taarifa zitolewe kwa wakati na kazi zifanyike. Kama huna jibu la swali la mteja mwambie ukweli na si kumsumbua au kumdanganya.Fanyeni kazi, acheni mambo ya kukaa ofisini, tokeni nje ili kujua shida za wananchi'' Alisema Mgandilwa.
Pia alisema kuwa Kigamboni
ni eneo pekee katika Jiji la Dar es Salaam linaloendelezwa, hivyo kuna haja ya
kupanga vizuri. Aliwaagiza watumishi wa ardhi
kusimami, kuzuia migogoro ya ardhi na kuuza kiwanja kwa watu wawili
tofauti.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni