Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Ally Mwalimu |
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu amekabidhi zaidi ya vitambulisho
2300 kwa wazee wa Manispaa ya Kigamboni kwa ajili ya kuwawezesha kupata
matibabu bila malipo katika hospitali zote za Manispaa ya Kigamboni.
Zoezi la utoaji vitambulisho
hivyo limefanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni ( Vijibweni) na
kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa manispaa ya kigamboni wakiongozwa na mkuu
wa Wilaya Mh. Hashim Mgandilwa.
Viongozi wengine waliohudhurio
hafla hiyo ni pamoja na Meya wa manispaa ya Kigamboni Mh.Maabad Suleiman Hoja
,Waheshimiwa madiwani pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni ndg Stephen
Katemba.
Akisoma risala mbele ya mgeni
Rasmi Ndg Katemba alisema wazee hao 2376 ni sehemu ya wazee 7000 wanaotarajiwa
kunufaika na mpango huo kwani mpaka sasa zoezi la kuwatambua linaendelea chini
ya usimamizi wa idara ya Ustawi na maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Kigamboni.
Mkurugenzi aliongeza kuwa
,kuanzia sasa hatarajii kuona wazee wakipata tabu ya matibabu kwani mpango huo
unawawezesha kupata matibabu yote bure kuanzia vipimo mpaka kumuona Daktari.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Ally Mwalimu akimkabidhi kitambulisho cha matibabu Mzee Jafary Said Said.
Picha ya pamoja |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni