Jumatatu, 12 Septemba 2016

Mkuu wa Wilaya akiongea na jumuia ya Mtaa wa Feri (Tandavamba)

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa amefanya mkutano na wamiliki wa Boti,wavuvi, mafundi friji,mafundi mashine za boti,mama lishe, wafanya biashara wa vioski, wauza maji na kahawa wa mtaa wa Feri (Tandavamba), lengo kuu likiwa ni kujitambulisha. Kutokana na mazingira mabaya ya sehemu wanayojipatia riziki umoja huo, Mgandilwa aliahidi kuwa litajengwa Soko la Kimataifa la Samaki ambalo pia litakuwa chanzo kikuu cha mapato katika Wilaya ya Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa akiongea na wakazi wa mtaa wa Feri - Tandavamba 

Mkurugenzi akiwa Tandavamba

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Bw. Stephen Katemba akijitambulisha kwa wakazi wa Mtaa wa Feri (Tandavamba) pia aliwaahidi kutekeleza yale yote yatakayoelekezwa na Mkuu wa Wilaya kwani yeye ndio Mtendaji katika Halmashauri.

Diwani wa Kata ya Kigamboni

Diwani wa Kata ya Kigamboni Mhe. Dotto Msawa akiwasalimia  wafanyabiashara wa Mtaa wa Feri (Tandavamba)  katika kikao cha Mkuu wa Wilaya hiyo alipoenda  kuwasalimia wananchi wa eneo hilo

Changamoto Sokoni


Utambuzi wa Mipaka ya Soko la Urassa



Mtendaji wa Kata ya Kigamboni Bw. Msafiri Munna (katikati) akionyesha mipaka ya soko la Urassa kwa timu ndogo iliyokuwa imeambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kigamboni Bw. Stephen Katemba (wapili kulia). Soko hili limezungukwa na majengo mbalimbali yakiwemo maduka na nyumba za kuishi


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ametembelea soko la Urassa

Jumapili, 11 Septemba 2016

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Bw. Stephen Katemba ameongea na watumishi wa Halmashauri hiyo mara baada ya kufika kuripoti katika Ofisi za Halmashauri zilizopo katika kata ya Mjimwema.  Bw. Katemba aliwapongeza sana watumishi kwa kukubali kufika Ofisini kuripoti na aliwaambia kuwa hiyo ni bahati na nafasi ya pekee kwao kwa kuteuliwa kuwa waanzilishi wa ofisi."Hongereni sana, hiyo ni opportunity kubwa ya kuanzisha ofisi mpya ya Kigamboni hivyo onyesheni ufanisi wenu.Mimi nawategemea sana, fanyeni kazi kwa bidii. Tunataka mabadiliko, hatutaki wafanyakazi wanaofanya kazi kwa kubabaisha, toa huduma kwa wakati na useme ukweli wakati wote. " Alisema Katemba.


Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Stephen Katemba(hayupo pichani) wakati akijitambulisha.








Ijumaa, 2 Septemba 2016

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar Es Salaam Bibi Theresia Mmbando (wa kwanza kulia) akiongea na watumishi wapya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni mara baada ya kuripoti Ofisini. Katibu Tawala aliwapongeza watumishi hao kwa kupata kituo kipya cha kazi na kuwaasa wafanye kazi kwa weledi na ufanisi wa hali ya juu.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Bw. David Mgonja akizungumza na Watumishi wapya wa Halmashauri ya Kigamboni kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar Es Salaam Bibi Theresia Mmbando. Watumishi hawa ni matokeo ya Mgawanyo wa watumishi wa Temeke Manispaa ambao baadhi yao wamehamishiwa Halmashauri ya Kigamboni

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Bw. David Mgonja (katikati) akimuonyesha Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar Es Salaam  Bibi Theresia Mmbando sehemu ya Ofisi ya Mkurugenzi

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa(Kushoto) akisalimiana na Bibi Theresia Mmbando Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar Es Salaam alipokwenda kuangalia ofisi mpya ya Wilaya ya Kigamboni